KANJA AWAHIMIZA VIJANA KUJIUNGA NA POLISI
Maelfu ya vijana wametakiwa kujitokeza kushiriki zoezi la usajili wa makurutu wa kujiunga na idara ya huduma za polisi NPS linalofanyika leo, zikiwa ni siku 2 baada ya mahakama kuonoa amri ya kusitisha zoezi hilo.
Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja, amesema makurutu 10,000 watasajiliwa katika zoezi hilo, akionya kuwa yeyote atakayejihusisha na ulaji au utoaji rushwa ili kushawishi usajili huo atakabiliwa kisheria.
Amelitaja zoezi hilo kuwa hatua muhimu ya kujenga kizazi kipya cha maafisa wa polisi watakaoendeleza mageuzi katika idara hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































