LEONARDO VARESE ALENGA NAFASI YA JUU SAFARI RALLY
Bingwa mara sita wa kitaifa wa magari ya daraja la Two-Wheel Drive (2WD), Leonardo Varese, analenga kumaliza katika nafasi tano bora kwenye uainishaji wa kitaifa katika mashindano ya Safari Rally Kenya, yatakayofanyika Naivasha kuanzia Machi 12 hadi 15.
Akiwa anaongozwa na msomaji ramani wake wa muda mrefu, Kigondu Kareithi, wawili hao watachuana kwa kutumia gari aina ya Toyota Yaris GR4 ambalo ni gari la kwanza la aina hiyo kushiriki mashindano nchini Kenya.
Varese atakuwa akishiriki Safari Rally kwa mara ya kwanza tangu irejee kwenye kalenda ya Mashindano ya Dunia ya Magari (WRC), na ameweka bayana kuwa analenga kuonyesha ushindani mkubwa katika kitengo cha kitaifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































