#Sports #Volleyball

AZMA YA GSU LIGI YA KVF INAPORUDI

Klabu ya voliboli ya GSU inaazimia kuweka nyuma masaibu yao katika ligi ya wanaume ya mchezo huo inayorejelewa hapo kesho ugani Kasarani Indoor Arena.

Mabingwa hao watetezi walikuwa na mwanzo duni, wakikosa kuandikisha ushindi katika mechi zao 2 za mkondo wa kwanza, ila kocha mkuu Gideon Tarus amesema wana matumaini ya kujikung’uta vumbi na kuwaonyesha wapinzani mtutu wa bunduki kwenye mkondo wa pili.

GSU walizabwa seti 3-2 na klabu ya KAPU licha ya kuchukua uongozi katika mechi ya ufunguzi, kabla ya kunyoroshwa na Trailblazers kwenye pambano la pili.

Walinda usalama hao hata hivyo wamepigwa jeki na kurejea kwa Hudson Kipchumba aliyekuwa amejiunga na Chema, pamoja na Felix Ouma, seta Abraham Wabwire na Douglas Cherop kutoka klabu ya polisi wa kitengo cha viwanja vya ndege, KAPU.

Mechi yao ya kwanza itakuwa dhidi ya NYS Ijumaa kabla ya kukabiliana na KDF Jumapili.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

AZMA YA GSU LIGI YA KVF INAPORUDI

WAKAZI WASHINIKIZA MWANGA UREJEE WEBUYE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *