KOCHA WA HARAMBEE STARLETS ASHUKURU MASHABIKI
Kocha mkuu wa Harambee Starlets, Beldine Odemba,
amewapongeza na kuwashukuru mashabiki wa timu hiyo baada
ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake
(WAFCON) 2026 litakalofanyika nchini Morocco.
Akizungumza mara baada ya ushindi wa bao 1–0 dhidi ya
Gambia kwenye mechi ya marudiano ya hatua ya mwisho ya
kufuzu iliyochezwa katika uwanja wa Stade Lat Dior mjini Thies,
Senegal, Odemba alisema ushindi huo ni kwa ajili ya taifa na
mashabiki waliowaamini.
Bao la Mwanahalima Adam dakika ya 56, lilihakikisha Starlets
wanarejea kwenye mashindano hayo kwa mara ya kwanza baada
ya miaka tisa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































