#Local News

MWENYEKITI WA IEBC ATOA ONYO KWA WAGOMBEA

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imetoa onyo kali kwa wagombea wa viti mbalimbali katika chaguzi ndogo zilizopangiwa kufanyika tarehe 27 mwezi huu, kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kuondolewa kwenye orodha ya wagombea iwapo watavuruga amani.

Akizungumza katika makao makuu ya IEBC hapa jijini Nairobi mwenyekiti wa tume hiyo Erastus Ethokon amekashifu visa vya utovu  wa nidhamu na vurugu hasa katika  maeneo bunge ya kasipul na mbeere kaskazini

Mkutano huo umewaleta pamoja viongozi wengine katika sekta ya usalama ikiwemo inspekta jenrali wa polisi Douglas Kanja na mwenyekiti wa tume ya kitaifa na uwiano na utangamano Samuel Kobia.

Imetayarishwa na Jones Koikai

MWENYEKITI WA IEBC ATOA ONYO KWA WAGOMBEA

NCIC: JAMII 5 ZINASHIKILIA 70% YA KAZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *