#Local News

OBURU ODINGA ATHIBITISHWA KUWA KIONGOZI WA ODM

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa imetoa tangazo la Gazeti Rasmi kuthibitisha maafisa wapya wa Chama cha ODM, huku Seneta wa Siaya Oburu Odinga akithibitishwa kuwa kiongozi mpya wa chama hicho.

Katika Gazeti Rasmi nambari 1157 la tarehe 19 Januari mwaka huu, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa imemtaja Oburu Odinga kama kiongozi wa chama, akichukua nafasi hiyo miezi kadhaa baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi wa ODM, hayati Raila Odinga.

Oburu amekuwa akihudumu kama kaimu kiongozi wa chama tangu kifo cha Raila na sasa amethibitishwa rasmi kushika wadhifa huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

OBURU ODINGA ATHIBITISHWA KUWA KIONGOZI WA ODM

RAIS AONGOZA UZINDUZI WA MRADI WA NYOTA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *