#Football #Sports

HAALAND AIREJESHA NORWAY KOMBE DUNIA

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Erling Haaland amelirejesha taifa lake la Norway katika dimba la kombe la dunia baada ya miaka 28, baada ya kufunga mara 2 katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya miamba walioporomoka Italia.

Haaland alifunga mabao hayo katika dakika ya 78 na 79, na kuzima kabisa ndoto ya Italia waliohitaji kuishinda Norway kwa angalau mabao 9-0 ili kumaliza wa kwanza kwenye kundi lao la I, na kuihakikishia timu yake ushindi katika mechi zote 8

Italia ambao walichukua uongozi wa mechi mwanzoni na kutamalaki kipindi cha kwanza, watalenga kufufua matumaini yao kupitia awamu ya mwondoano, wakilenga kujiondolea aibu ya kukosa dimba hilo mara 3 mtawalia.

Mara ya mwisho kwa Norway kushiriki kombe la dunia ulikuwa mwaka wa 1998, babake Haaland, Alf Inge, akiwa sehemu ya kikosi hicho na sasa mwanawe ameirejesha timu hiyo miaka 28 baadaye.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

HAALAND AIREJESHA NORWAY KOMBE DUNIA

KOMBE LA DUNIA: DR CONGO YAWEKA HAI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *