WANDANI WA KINDIKI WATETEA ‘TONGE’
Mjadala kuhusu ni nani atakayekuwa naibu rais wa Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao umeendelea kushika kasi huku wandani wa naibu Rais wa sasa Kithure Kindiki wakisisitiza kuwa wadhifa huo hautapokonywa Kindiki.
Wakizungumza kwenye mkutano mjini Embu wakiwa wameandamana na Kindiki, wandani hao wamemtaka kinara wa ODM Oburu Oginga kukoma kukimezea mate kiti hicho.
Naye Kindiki amewahimiza viongozi kutuliza joto la kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































