JOHO AAHIDI USHIRIKISHWAJI WA UMMA KUHUSU UCHIMBAJI WA DHAHABU IKOLOMANI
Waziri wa Madini na Uchumi wa Baharini Ali Hassan Joho, amesema wizara yake itawahusisha wananchi katika mazungumzo ya kutatua mzozo unaoendelea kuhusu mpango wa uchimbaji wa dhahabu eneo la Ikolomani, kaunti ya Kakamega.
Akizungumza baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano na serikali ya kaunti ya Kakamega, Joho amesema ushirikiano wa karibu kati ya serikali kuu, kaunti na jamii ni muhimu ili kufikia mwafaka wenye manufaa kwa wote.
Aidha Joho Amesisitiza kuwa maslahi ya wakazi yatapewa kipaumbele, hasa katika suala la fidia, akiahidi kuwa hakuna mradi utakaotekelezwa bila ridhaa na ulinzi wa haki za jamii ya eneo hilo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































