#Football #Sports

JUNIOR STARS WAANZA KAMPENI YA AFCON

Timu ya taifa ya soka ya vijana wasiozidi umri wa miaka 17 Junior Stars wataanza safari yao ya kufuzu mashindano ya AFCON U17 ukanda wa CECAFA dhidi ya Somalia hii leo, wakilenga kuibuka na ushindi katika mechi yao ya ufunguzi nchini Ethiopia.

Stars wamewekwa kwenye kundi A Pamoja na wenyeji Ethiopia, Rwanda, South Sudan na Somalia, Ethiopia wakiwa kileleni kwa pointi 3 baada ya kuvuna ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rwanda, huku Somalia na South Sudan wakiwa na pointi 1 kufuatia sare ya magoli 2 kwenye mechi yao za ufunguzi.

Mechi ya pili ya Junior Stars itakuwa Ijumaa dhidi ya Rwanda, kabla ya kushuka dimbani dhidi ya South Sudan na kumaliza mechi za makundi dhidi ya Ethiopia.

Timu 2 za kwanza zitapata fursa ya kushiriki kipute cha taifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 AFCON U17.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

JUNIOR STARS WAANZA KAMPENI YA AFCON

THUNDER WALENGA KUNGURUMA BAL ELITE 16

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *