10 WAFARIKI KWENYE AJALI NAIVASHA
Idadi ya waliofariki kwenye ajali ya barabara karibu na Karai eneo la Naivasha usiku wa kuamkia leo imepanda hadi 10 huku watu wengine 5 wakiwa katika hali mahututi.
Ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Greenline lililokuwa likielekea Nairobi na matatu iliyokuwa ikielekea Nakuru, polisi wakisema 8 kati ya waathiriwa walikuwa abiria wa matatu na 2 kwenye basi akiwemo mtoto mchanga.
Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Naivasha Wilson Sigei amesema dereva wa basi alijaribu kupita gari jingine kabla ya kutokea kwa ajali hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































