#Business

NTSA YAONYA KUHUSU MAJUKWAA YA ULAGHAI

Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama barabarani (NTSA) imeonya umma kuhusu tovuti ghushi, Mverified, ambayo inatoa nakala za Rekodi za magari kwa uwongo na huduma za utafutaji kwenye daftari.

NTSA imefafanua kuwa tovuti hiyo haihusiani na mamlaka hiyo na ikahimiza yeyote aliyelaghaiwa kuripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu.

Kufuatia ripoti,shirika hilo lilisisitiza kuwa utafutaji rasmi wa COR na kitabu cha kumbukumbu unapatikana tu kupitia tovuti ya huduma ya NTSA kwenye eCitizen, na kugharimu Ksh550 kwa kuchakatwa papo hapo.

Tovuti ya ulaghai ilitoza Ksh920 na kuelekeza malipo kwa akaunti ya kibinafsi, ikidai kutuma hati kupitia barua pepe au SMS.

NTSA imetoa tahadhari hiyo baada ya Mkenya mmoja kuibua wasiwasi mtandaoni, ikibaini kuwa ulaghai huo huongezeka haswa mwishoni wa mwaka wakati shughuli za magari zinapoongezeka.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *