MATIBABU YAENDELEA KUSAMBARATIKA NAIROBI, MARSABIT
Wakazi katika kaunti za Nairobi na Marsabit wanaendelea kutatizika kupata huduma za matibabu kwenye hospitali za umma kutokana na mgomo wa wahudumu wa afya, wanaosema hali imedorora zaidi na kuweka maisha ya wagonjwa hatarini.
Kulingana na maafisa wa muungano wa wahudumu hao wakiongozwa na viongozi wa KUCO, takribani asilimia 90 ya huduma sasa hazipatikani, huku serikali za kaunti hizo mbili zikikosa kushughulikia matakwa yao.
Maafisa wa maabara na kliniki katika kaunti ya Marsabit wamekuwa kwenye mgomo kwa siku 115.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































