NDAKWA AAHIDI USHIRIKIANO
Mbunge mteule wa Malava kaunti ya Kakamega David Athman Ndakwa, ameahidi kuwashirikisha wakazi wote eneo hilo katika uendeshaji wa majukumu yake, bila kuzingatia tofauti za kisiasa.
Akizungumza baada ya kupokezwa cheti cha ushindi kwenye uchaguzi mdogo, Ndakwa ameipongeza IEBC akisema imeendesha uchaguzi huo kwa mujibu wa mwongozo wa sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































