#Football #Sports

CITY WAWATOA MADRID RANGI

Manchester City walitoka nyuma na kutia madoa kwenye rangi nyeupe ya Real Madrid, kwa kuwapokeza kichapo cha magoli 2-1 ugani Santiago Barnabeu jijini Madrid katika kipute cha ligi ya klabu bingwa barani Ulaya.

Kichapo hicho kimemwacha kocha mkuu wa Madrid Xabi Alonso katika njia panda kuhusiana na kibarua chake, ambacho huenda kikamponyoka muda wowote kutokana na matokeo duni katika mashindano yote baada ya kuwaongoza miamba hao kwa miezi 6.

Los Blancos waliokosa huduma za Kylian Mbappe, walichukua uongozi kunako dakika ya 28 kupitia kwa Rodrygo, ila uongozi wao ukafutwa dakika 7 baadaye kupitia kwa beki wa kushoto Nico O’Reilly.

Erling Haaland aliwapa City uongozi kupitia mkwaju wa Penalti, baada ya beki Antonio Rudiger kumkamata na kumweka chini wakati wa mkwaju wa kona kabla ya kutamatika kwa kipindi cha kwanza.

Ushindi huo umewapandisha City hadi nafasi ya 4, zikiwa zimesalia mechi 2 zitakazochezwa mwaka ujao huku Real Madrid sasa wakiwa katika nafasi ya 7.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CITY WAWATOA MADRID RANGI

ARSENAL WADUMISHA REKODI UEFA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *