MGOMO WA MADAKTARI MOMBASA WASITISHWA
Maafisa wa Union KMPDU wakiongozwa na Katibu Mkuu Davji Atellah, wamesitisha mgomo wa madaktari katika kaunti ya Mombasa hatua inayokuja baada ya mazungumzo ya saa nne yaliyofanyika katika ofisi ya Gavana wa Mombasa.
Uamuzi huo umefikiwa kufuatia kikao kati ya viongozi wa muungano huo na Gavana wa Mombasa, Abdulswamad Sharif Nassir, ambapo pande zote zilijadili masuala yaliyokuwa yameibua mvutano.
KMPDU imesema mazungumzo hayo yalikuwa ya kujenga na yamefungua njia ya kutatua changamoto zilizokuwa zimeorodheshwa na madaktari.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































