WANAFUNZI 10 HOSPITALINI KUFUATIA AJALI KIMENDE
Wakati uo huo, wanafunzi 10 wa shule ya Bishop Okoth wamepelekwa katika hospitali ya kimisheni ya Kijabe kwa matibabu baada ya basi lao kuanguka katika eneo la Kimende kaunti ndogo ya Naivasha.
Imearifiwa kwamba basi hilo lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi 46, lilikosa mwelekeo na kutoka nje ya barabara kuu ya Nairobi- Nakuru kabla ya kuanguka.
Walioshuhudia wamehusisha ajali hiyo na uchovu wa dereva ingawa uchunguzi unaendelea.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































