PIGO LA MAJERAHA KATIKA SAFU YA ULINZI YA ARSENAL
Ligi kuu ya soka nchini Uingereza EPL inarejea wikendi hii huku viongozi Arsenal wakikabiliwa na uwezekano wa kukosa huduma za mabeki Gabriel Magalhaes, Jurrien Timber na Riccardo Calafiori kutokana na majeraha waliyopata katika majukumu ya kimataifa.
Arsenal ambao wamekuwa na ngome imara ya ulinzi Barani Ulaya msimu huu wakienda mechi 8 bila kufungwa bao, watamenyama katika debi ya London na Tottenham Hotspurs Jumapili hii, bila huduma za wachezaji hao.
Timber alipata jeraha la goti katika ushindi wa mabao 4-0 wa timu yake ya taifa ya Uholanzi dhidi ya Lithuania.
Naye Magalhaes ambaye ushirikiano wake na William Saliba umekuwa bora zaidi kwa misimu kadhaa, aliumia kwenye mechi ya kirafiki baina ya Brazil na Senegal, na anahofiwa kukaa nje hadi Januari.
Calafiori ambaye amekuwa kiungo muhimu kama fulbeki wa kushoto katika nyingi ya mechi za the Gunners, alijiondoa katika kikosi cha Italia akiwa na jeraha la paja, ingawa taarifa zimearifu kuwa huenda akawa kikosini Jumapili.
Arsenal tayari wana majeruhi ambao ni fowadi Viktor Gyokeres, Gabriel martinelli, Kai Havertz na Noni Madueke, na ombi litakuwa ni kurejea kwa mabeki wao 3 katika uwindaji wa ligi msimu huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































