#Local News

BRIAN ODHIAMBO: MAAFISA WA KWS KUJITETEA

Familia ya mvuvi Brian Odhiambo, aliyetoweka mapema mwaka jana katika mbuga ya kitaifa ya Wanyama ya Lake Nakuru imeelezea kupata afueni baada ya mahakama ya Nakuru kuamuru kwamba maafisa wa KWS wanaohusishwa na kutoweka kwa mvuvi huyo, wana kesi ya kujibu.

Kwenye uamuzi wake, hakimu wa mahakama hiyo Kipkurui Kibellion, amesema kuwa ushahidi uliowasilishwa unatosha kwa sita hao kujibu mashtaka ya utekaji nyara, kesi hiyo ikiratibiwa kuanza kusikilizwa mwezi Juni mwaka huu.

Maafisa hao ni Alexander Lorogoi, Francis Wacira, Michael Wabukhala, Isaac Ochieng, Abdulrahaman Sudi na Evans Kimaiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

BRIAN ODHIAMBO: MAAFISA WA KWS KUJITETEA

REJESHA EDUAFYA, SERIKALI YATAKIWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *