MGOGORO MPYA WANUKIA UON
Huenda shughuli za masomo zikayumbishwa tena katika chuo kikuu cha Nairobi iwapo serikali haitatekeleza matakwa ya wahadhiri chuoni humo, ikiwemo kutia saini na kutekelezwa kwa mkataba wa maelewano wa pamoja CBA.
Katika kikao na waandishi wa habari, wahadhiri kupitia muungano wa UASU wameilaumu serikali kutokana na kucheleweshwa kwa mkataba huo, na madai kwamba serikali inavuruga mpango wa kuwaajiri wafanyakazi katika chuo hicho.
Mgogoro huo mpya unanukia miezi michache baada ya baraza jipya kuteuliwa ili kutatua mgogoro wa uongozi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































