LUIS ENRIQUE ATABIRI CHANGAMOTO KWA PSG LIGUE 1
Kocha wa Paris Saint-Germain, Luis Enrique, amesema anatarajia timu yake kukumbwa na ushindani mkali katika miezi ya mwisho ya msimu wa Ligue 1, akianza na mechi dhidi ya wapinzani wao wakuu Marseille itakayochezwa Jumapili.
PSG, ambao ni mabingwa wa Ulaya, wameshinda mechi zao sita za mwisho za ligi, lakini bado wanakabiliwa na presha ya kutwaa taji hilo kutokana na changamoto isiyotarajiwa kutoka kwa Lens.
Lens wako pointi mbili pekee nyuma ya PSG kwenye msimamo wa ligi, na pia wamefanikiwa kufuzu robo fainali ya Kombe la Ufaransa katikati ya wiki, hali inayozidisha ushindani katika mbio za ubingwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































