KATASI ANG’ARA LIGI KUU YA KPL
Kipa wa AFC Leopards, Humphrey Katasi, ameendelea kuwa tegemeo muhimu kwa timu hiyo katika msimu uliogubikwa na ushindani mkali.
Akiwa na mechi 10 bila kuruhusu bao, Katasi anaongoza orodha ya makipa wenye mechi nyingi safi katika SportPesa Premier League na yuko katika nafasi nzuri ya kuwania tuzo ya kipa bora wa msimu.
Katasi anaongoza kwa tofauti ya mechi mbili dhidi ya wapinzani wake wa karibu, Job Ochieng na Stephen Otieno, ambao kila mmoja ana mechi tisa bila kuruhusu bao.
Makipa wengine wanaomfuatia kwa karibu ni Allan Ngeleka, Byrne Omondi, na Kevin Ouru, kila mmoja akiwa na mechi nane safi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































