POLICE FC WATEGEMEA UAMUZI WA CAF
Klabu ya Al Hilal Omdurman imepuzilia mbali madai ya Police FC ya Kenya kwamba klabu hiyo ya Sudan iliwachezesha wachezaji wasiofaa katika mkondoo wa pili wa kufuzu awamu ya makundi ya mashindano ya klabu bingwa barani Afrika.
Kwenye taarifa, Omdurman ambayo iliwabandua Police FC, imeyataja madai hayo kuwa yasiyo na msingi.
Miongoni mwa malalamishi ambayo Police FC imewasilisha kwa shirikisho la soka barani Afrika ni hatua ya Omdurman kuwajumuisha wachezaji 13 wa kigeni kikosini, ilhali shirikisho la soka nchini Sudan linaziruhusu klabu zake kuwasajili wachezaji 10 pekee wa kigeni.
Baadhi ya wachezaji wanaolalamikiwa ni kipa Soufian Farid Ouédraogo kutoka Burkina Faso, mshambulizi wa Nigeria Sunday Damilare Adetunji, aliyefunga mara 2 katika mechi ya marudiano, na beki wa DR Congo Ernest Luzolo, Police ikisema watatu hao hawakuwa wamesajiliwa na shirikisho la soka nchini Sudan.
Iwapo CAF itakubaliana na Police FC, Al Hilal Omdurman itapokonywa nafasi yake katika awamu ya makundi na kukabidhiwa Police FC.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































