#Business

EPRA YATANGAZA BEI ZA MAFUTA KUSALIA ZILIVYO

Mamlaka ya kudhibiti wa kawi Petroli (EPRA) imetangaza kuwa bei za mafuta hazitabadilika kati ya tarehe 15 mwezi hu una januari 14.

Kwa mwezi wa tatu mfululizo, mdhibiti ametangaza bei za pampu za rejareja za Super Petrol kuwa shilingi 184.52, Dizeli kuwa shilingi 171.47, na Mafuta ya Taa kuwa Ksh154.78, mtawalia, jijini Nairobi. Bei za hivi punde za pampu zinajumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani ya asilimia 16 (VAT) kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Fedha ya 2023, Sheria ya Kodi (Marekebisho) ya Sheria ya 2024 na viwango vilivyorekebishwa vya ushuru wa bidhaa vilivyorekebishwa kwa mfumuko wa bei kulingana na Ilani ya Kisheria ya 2024.

Jijini Mombasa, bei ya pampu iko chini kidogo kwa mwezi huu, huku petroli ikitarajiwa kuuzwa kwa Ksh181.24, huku dizeli ikiuzwa kwa Ksh161.19. Mafuta ya taa, yatauzwa kwa Ksh151.49. Katika, mji  wa Nakuru, petroli  itauzwa kwa Ksh183.56, huku dizeli ikiuzwa kwa Ksh170.87. Mafuta ya taa yatauzwa Ksh154.21.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

EPRA YATANGAZA BEI ZA MAFUTA KUSALIA ZILIVYO

CITY MGONGONI PA ARSENAL EPL

EPRA YATANGAZA BEI ZA MAFUTA KUSALIA ZILIVYO

28 WAJERUHIWA KWENYE AJALI NAKURU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *