GACHAGUA AITAKA MAREKANI ‘KUCHEZA KIVENEZUELA’
Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua ametoa wito kwa serikali ya Marekani kuharakisha uchunguzi unaoendelea katika Sakata ya ulaghai kupitia mpango wa kuwasaidia Watoto wasiojiweza katika jimbo la Minnesota, akisema sehemu ya mapato ya ulaghai huo ilifadhili kampeni za Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Gachagua ameitaka Marekani kuwafuatilia wahusika, akidai baadhi yao wanalindwa na serikali ya Kenya kupitia amri za mahakama, akitaka mbinu zilizotumika kumkamata Rais wa Venezuela Nicholas Maduro kutumika.
Mamilioni ya dola ziliripotiwa kufujwa kupitia mpango huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































