MASWALI KUHUSU MAN UNITED
Katika mtindo wa hatua moja mbele, hatua moja nyuma, klabu ya Manchester United ilionyesha kuimarika ilipoicharaza Wolves mabao 4-1 katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza jana usiku ugani Molineux.
Swali linaloulizwa ni iwapo ushindi huo ni mwamko mpya au ni kwa sababu walipata Wolves yenye masaibu chungu nzima ikiwa ya mwisho kwenye ligi hiyo na pointi 2 pekee baada ya mechi 15.
Ushindi mnono dhidi ya Crystal Palace ulifuatwa na sare dhidi ya West Ham United ambao pia wana fomu mbovu msimu huu, na kabla ya hapo, ushindi katika mechi 3 mfululizo ulifuatwa na msururu wa mechi 3 bila ushindi, kabla ya kuadhibiwa nyumbani na Everton goli 1-0
Ushindi wa jana ni mkubwa wa United msimu huu, na hawajawahi kupata ushindi mkubwa zaidi ya huo tangu ujio wa kocha mkuu Ruben Amorim miezi 13 iliyopita.
Amorim amekiri kuwa Wolves wako katika fomu mbovu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































