UPINZANI WADAI NJAMA YA KUWAHONGA WAPIGA KURA
Muungano wa upinzani umeibua madai kuhusu kuhongwa kwa wapiga kura katika maeneo yanayojiandaa kwa chaguzi ndogo wiki ijayo ambako wagombeaji wa upinzani wanamenyana na wenzao wanaoegemea serikali ya Kenya Kwanza.
Katika kikao na wanahabari, muungano huo ukiongozwa na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka umesema wapiga kura wameahidiwa hadi shilingi 5,000 iwapo watathibitisha kwamba wamewapigia kura wagombeaji walio upande wa serikali.
Wameitaka IEBC kuchukua hatua za mapema.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































