VIONGOZI WAONYA DHIDI YA KUVURUGA ZIARA YA RUTO
Baadhi ya viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Kakamega wamehimiza ushirikiano wa viongozi wote katika kaunti hiyo wakati wa ziara ya Rais William Ruto, wakisema hatua hiyo itahakikisha wanafaidika pakubwa kutokana na ziara hiyo.
Rais amerataibiwa kuzuru maeneo kadhaa ya kaunti hiyo kuzindua miradi ya maendeleo, huku madai yakiibuka kwamba kuna njama ya vijana kutumiwa kutatiza mkutano wa rais.
Nabii Nabwera ni mbunge wa Lugari.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































