#Football #Sports

WOLVES WAMNG’ATA KOCHA WAO PEREIRA

Klabu ya Wolves inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza EPL imempiga kalamu meneja mkuu Vitor Pereira baada ya kushindwa kushinda mechi hata moja katika mechi 10 za ufunguzi wa msimu.

Pereira aliyetia Saini mkataba wa miaka 3 na kalbu hiyo mwezi Sptemba baada ya kuwaongoza Wanderers kuepuka kushushwa daraja msimu jana, aliandikisha pointi 2 pekee na Wolves katika mechi 10.

Msumari wa mwisho kwenye jeneza ulitiwa na kichapo cha mabao 3-0 mikononi mwa Fulham Jumamosi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *