#Football #Sports

AFCON YABISHA

Mashindano ya Kombe la Mataifa bingwa barani Afrika, AFCON, yanaanza rasmi Jumapili hii nchini Morocco, yakishirikisha mataifa 24 kutoka bara hili.

Wenyeji Morocco, ambao ndio washindi wa AFCON mwaka 1976, wanalenga kukata kiu cha kusubiri taji hilo kwa zaidi ya miaka 40, wakilenga kutumia faida ya uwanja wa nyumbani watakapoanza kampeni yao kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Comoros.

Mabingwa watetezi Ivory Coast, ambao wamewahi kushinda taji la AFCON mara tatu—mwaka 1992, 2015 na 2023—wataanza kampeni ya kutetea ubingwa wao dhidi ya Mozambique.

Mashindano haya yamegawanywa katika makundi sita, kuanzia Kundi A hadi F, kundi F likitajwa kuwa miongoni mwa makundi yenye ushindani mkubwa zaidi kwa kuwa linajumuisha timu zenye historia tofauti kwenye AFCON.

Katika kundi hilo, Cameroon imewahi kushinda AFCON mara tanoIvory Coast mara tatu, huku Gabon na Mozambique zikiwa hazijawahi kushinda taji hilo lakini zina uzoefu wa kushiriki mashindano ya bara.

Mataifa mengine yenye rekodi kubwa kwenye AFCON ni Misri, bingwa mara sabaNigeria mara tatu, na Senegal bingwa mara moja, mwaka 2021.

Waandalizi wamesema maandalizi ya viwanja, usalama na miundombinu iko tayari kwa mechi za ufunguzi.

Mashindano ya AFCON yanatarajiwa kuendelea kwa wiki kadhaa yakileta burudani, ushindani na mshikamano wa mataifa ya Afrika.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

AFCON YABISHA

POLICE FC WATIWA PINGU

AFCON YABISHA

NTSA YAWAONYA MADEREVA KUHUSU ULAGHAI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *