RAIS RUTO ASIFU USHINDI WA WA DAVID MUNYUA KWENYE DARTS
Rais William Ruto amepongeza ushindi wa kihistoria wa David Munyua katika Mashindano
ya Dunia ya Darts ya Paddy Power 2025/26, ushindi uliotikisa taifa na kuzua fahari kubwa ya
kitaifa.
Munyua ambaye ni daktari wa mifugo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Murang’a,
aliandika historia baada ya kuwa Mkenya wa kwanza kushiriki na kushinda mechi katika
mashindano hayo maarufu yaliyofanyika Alexandra Palace jijini London.
Katika mechi yake ya kwanza kabisa kwenye mashindano hayo, Munyua alisababisha
mshtuko mkubwa kwa kumshinda mchezaji nambari 18 duniani na bingwa wa zamani wa
World Grand Prix, Mike De Decker wa Ubelgiji, kwa seti 3-2.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































