HOFU YA AJALI BARABARANI
Hofu imeibuka nchini kuhusu ajali za barabarani, zaidi ya watu 20 wakiaga dunia kwenye ajali hizo katika kipindi cha siku 5 za mwanzo wa mwaka huu pekee huku wito ukitolewa kwa madereva kuwa makini.
Hii ni baada ya watu 9 kufariki kwenye ajali katika eneo la Naivasha hapo jana na wengine 55 kujeruhiwa, ajali ambayo imehusishwa na uchovu wa dereva mbali na kuhudumu kwa saa nyingi bila kupumzika.
Waziri wa uchukuzi Davis Chirchir, na kamanda wa polisi eneo la Naivasha Wilson Sigei, wamewataka madereva kuchukua tahadhari.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































