#Local News

SERIKALI YAAGIZWA KUMLIPA CRITICOS 30M

Mahakama kuu imeiagiza serikali kumlipa fidia ya shilingi milioni 30 mbunge wa zamani wa Taita Taveta Basil Criticos baada ya kubaini kuwa haki za kikatiba kuhusu umiliki wa mali za kiongozi huyo zilikiukwa.

Kwenye uamuzi wake, mahakama imesema kuwa Criticos alinyimwa haki haki zake za kikatiba kinyume na kipengee cha 40 cha katiba, kinachompa kila mkenya haki ya kumiliki mali.

Kulingana na Criticos, maelfu ya watu walivamia shamba lake na kuharibu mikonge kati ya mwaka 1998 na 2000 huku maafisa wa serikali wakikosa kuwaondoa licha ya kilio chake.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SERIKALI YAAGIZWA KUMLIPA CRITICOS 30M

JOHO AWE NAIBU WA RUTO, VIONGOZI WA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *