STARLETS UFARANSA KWA MAZOEZI
Kikosi cha wanawake wa timu ya taifa ya soka Harambee Starlets kitacheza mechi 2 za kirafiki dhidi ya Benin na Ivory Coast, na kisha kufanya kambi ya mazoezi nchini Ufaransa.
Haya ni katika maandalizi ya dimba la taifa bingwa barani Afrika kwa wanawake, WAFCON 2026, litakaloandaliwa mwezi ujao nchini Morocco.
Rais wa shirikisho la soka nchini, FKF, Hussein Mohammed, amesema kikosi hicho kitaelekea Kusini mwa Ufaransa katika eneo la Miramas kwa kambi baada ya mechi hizo.
Mechi hizo za kirafiki zitachezwa katika uwanja wa Alassane Ouattara jijijini Abidjan, Ivory Coast, mwanzo tarehe 4 dhidi ya Benin kabla ya wenyeji baadaye tarehe 6 mwezi ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































