MAHAKAMA YA MURANG’A YAHOFIA MSONGAMANO KWENYE MAGEREZA
Mahakama kuu ya Murang’a imeagiza kuimarishwa kwa utendakazi kupitia mageuzi ya kidijitali hii ni kufuatia msongamano unaozidi kuongezeka katika magereza mbalimbali katika kaunti hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla ya kutoa kompyuta na tarakilishi kwa gereza la maranjau jaji wa mahakama kuu ya Murang’a Cecilia Githua amesema mpango huo utahakikisha haki inatendeka kwa njia bora kwa kila mfungwa.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































