MIKAKATI YA RBA YA KULINDA PENISHENI
Mamlaka ya Mafao ya Kustaafu (RBA) imeanzisha mikakati mipya ya kukabiliana na ongezeko la tatizo la michango ya pensheni isiyolipwa, ikiwa ni pamoja na adhabu kali na hatua zinazoweza kuzuia taasisi zinazokiuka sheria kupata fedha za serikali.
Chini ya mageuzi hayo, Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) itachukua jukumu kuu katika kufuatilia na kurejesha michango ya pensheni ambayo haijalipwa. Kulingana na data ya RBA, makato ya pensheni ambayo yalikusanywa lakini hayakutumwa kwa mipango ya kustaafu yalifikia jumla ya shilingi bilioni 72 kufikia Juni 2025, kutoka shilingi bilioni 57 mwaka uliotangulia, kuashiria ongezeko la asilimia 26.31.
Nyingi ya michango hiyo ambayo haijalipwa, karibu asilimia 98, inahusishwa na serikali za kaunti, vyuo vikuu vya umma visivyo na pesa taslimu, viwanda vya sukari, na mashirika mengine ya serikali.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































