MAHAKAMA KUAMUA OMBI LA DHAMANA KWA ‘WEZI WA KIFAHARI’
Washukiwa 6 wa msururu wa wizi unaoelenga majumba katika mitaa ya kifahari jijini Nairobi na viunga vyake watabaini hatma yao kuhusu ombi la dhamana hapo kesho baada ya upande wa mashtaka kuomba wazuiliwe kwa siku 21 moja ili ukamilishe uchunguzi dhidi yao.
6 hao waliokamatwa na maafisa wa DCI baada ya kuvunja nyumba moja mtaani South B, walifikishwa katika mahakama ya Makadara hapo jana, mawakili wao wakipinga ombi la upande wa mashtaka.
Kwa mujibu wa idara ya DCI, washtakiwa wanahusishwa na visa vingine vya wizi katika maeneo mbali mbali ya taifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































