GRIEZMANN AANZA MAZUNGUMZO NA ORLANDO CITY
Mshambuliaji Wa Ufaransa, Antoine Griezmann, anaripotiwa kufanya mazungumzo na klabu ya Orlando City SC inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka ya Marekani.
Kwa sasa Griezmann anakipiga katika klabu ya Atlético Madrid, ambako ndiye mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo. Pia alifunga mabao 44 katika maisha yake ya kimataifa akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na uwezekano wa kuhamia Marekani, akijulikana kuwa shabiki wa ligi mbalimbali za huko ikiwemo mpira wa kikapu na NFL.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































