MSAADA WA AMBULENSI KUTOKA WHO
Huduma za matibabu nchini zimepigwa jeki kufuatia msaada wa ambulensi 14 za kisasa na dawa zenye thamani ya shilingi milioni 350 kwa serikali kutoka shirika la Afya duniani WHO kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa umma nchini.
Walengwa katika msaada huo ni akina mama wajawazito na Watoto wanaozaliwa, Rais William Ruto akizitaka hospitali kutoa takwimu za akina mama wanaofariki wakati wa kujifungua na Watoto wachanga.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































