#Football #Sports

CHELSEA YASAKA ‘MRITHI’ WA MARESCA

Klabu ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza EPL inalenga kupata huduma za meneja wa klabu ya ADC Bournemouth Andoni Iraola huku meneja wa sasa Enzo Maresca akiendelea kujipata chini ya shinikizo.

Shinikizo za hivi punde zimetokana na the Blues kupokezwa kichapo cha mabao 2-1 mikononi mwa Sunderland, ripoti zikiibuka kwamba maafisa wakuu kwenye klabu wameanza kujadili mikakati ya kuifufua klabu yao ikiwemo kumtimua Maresca.

Miongoni mwa hofu ni mfumo wa mashambulizi na matokeo yasiyoridhisha, na kwamba usimamizi wa klabu sasa haumuungi mkono Maresca kikamilifu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Caught Offside, Iraola ni miongoni mwa makocha wanaowindwa ili kuinoa Chelsea.

Bournemouth yake Iraola ni miongoni mwa klabu ambazo zimewashangaza wengi msimu huu, ikiwa katika nafasi ya 2 kwenye msimamo wa ligi, pointi 4 pekee nyuma ya viongozi Arsenal.

Ufanisi wa raia huyo wa uhispania kwa bajeti ndogo umevutiqa klabu nyingine kama vile Manchester United na Juventus.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CHELSEA YASAKA ‘MRITHI’ WA MARESCA

GOR WATANGAZA KUREJEA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *