#Sports

DEAFLYMPICS 2025 KUFUNGA MILANGO LEO

Mashindano ya riadha kwa wachezaji wasio na uwezo wa kusikia Summer Deaflympics 2025 yameratibiwa kukamilika rasmi hii leo jijini Tokyo Japan, Kenya ikihitimisha safari yake kwa medali 15.

Medali ya mwisho kwa Kenya ilikuwa nishani ya fedha, baada ya David Kipkogei kumaliza katika nafasi ya 2 kwenye mbio za marathon ya wanaume, akiandikisha muda wa saa 2:16.10, mbele ya Jose Libardo wa Colombia na nyuma ya mshindi wa dhahabu Otto Kingsedt wa Sweeden.

Kenya imemaliza na medali 15 kwa jumla, zikiwemo dhahabu 5, fedha 6 na shaba 4

Ukraine imeongoza kwenye mashindano hayo baada ya kujizolea jumla ya medali 100.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

DEAFLYMPICS 2025 KUFUNGA MILANGO LEO

JUNIOR STARS WAJIANDAA KUIVAA ETHIOPIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *