#Local News

14 WAAGA, 16 WAJERUHIWA KWENYE AJALI WEBUYE

Watu 14 wameaga dunia huku wengine 16 wakiachwa na majeraha usiku wa kuamkia leo baada ya kugongwa na trela karibu na eneo la Malaha kwenye barabara kuu ya Webuye kuelekea Kitale.

Kwa mujibu wa OCPD wa Webuye Rosemary Odeke, 14 hao waliaga dunia papo hapo baada ya kugongwa na trela hiyo, ripoti zikionyesha kuwa umati ulikuwa umekusanyika eneo hilo kushuhudia ajali ya awali iliyokuwa imehusisha gari jingine na mhudumu wa boda boda.

Majeruhi wamelazwa katika hospitali ya rufaa mjini Webuye, huku walioaga pia wakipelekwa katika hifadhi ya hospitali hiyo wanakosubiri upasuaji na kutambuliwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *