#Football #Sports

RAUNDI YA 4 YA CARABAO KUMALIZIKA LEO

Kipute cha Carabao kinaendelea hii leo katika raundi ya 4 huku jumla ya mechi 9 zikisakatwa.

Mabingwa watetezi Newcastle United watakuwa wenyeji wa Tottenham, Arsenal vs Brighton, Man City wakiwatembelea Swansea City nao Wolves wamalize udhia dhidi ya Chelsea ugani Molineux.

Crystal Palace watakuwa wageni wa Liverpool, wakiwa tayari wamepambana mara 2 msimu huu, Palace wakiibuka na ushindi katika Community Shield na katika ligi kuu, na watalenga kuwalaza mabingwa hao wa EPL kwa mara ya 3 msimu huu.

Kwenye kambi ya Arsenal, huenda wakakosa huduma za wachezaji Saliba, Declan Rice, Riccardo Calafiori na Gabriel Martinelli kutokana na majeraha.

Katika matokeo ya hapo jana, safari ya Grimsby Town walioibandua Manchester United katika raundi ya 2 ilitamatika baada ya kucharazwa mabao 5:0 na Brenford.

Fulham walifuzu raundi ya 5 baada ya kuwabandua Wycombe kwa mabao 5-5 kupitia mikwaju ya penalti kufuatia sare ya bao 1:1

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

RAUNDI YA 4 YA CARABAO KUMALIZIKA LEO

POLICE FC WATEGEMEA UAMUZI WA CAF

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *