KANG’ATA AWATAKA WAKENYA KUKATAA SIASA ZA MGAWANYIKO
Viongozi wa kisiasa wamewataka Wakenya kususia siasa za kugawanya taifa na badala yake kuhimiza umoja na ustawi wa pamoja.
Akizungumza katika hafla ya mchango eneo la Seme, kaunti ya Kisumu, gavana wa Murang’a Irungu Kang’ata amesema siasa za uchochezi wa kikabila zimeendelea kudhoofisha maendeleo katika maeneo mengi nchini.
Kang’ata amesisitiza kuwa wakati umefika kwa wananchi na viongozi kuelekeza nguvu katika ajenda zinazoinua maisha ya watu, kama kuboresha uchumi, elimu na huduma za afya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































