#Local News

MAHAKAMA YARUHUSU UTEUZI WA BODI YA UAJIRI BUNGOMA

Bodi ya uajiri wa umma katika kaunti ya Bungoma imepata afueni baada ya mahakama ya ajira na leba mjini Bungoma kutupilia mbali kesi iliyokuwa imewasilishwa kupinga uteuzi wa wanachama kuhudumu kwenye bodi hiyo.

Kwenye uamuzi katika kesi iliyowasilishwa na mwanasiasa Rodgers Siboe ambaye hakuorodheshwa baada ya kutuma maombi, jaji David Nderitu ameamuru kuwa mwanasiasa huyo hafuzu kuhudumu kwenye bodi hiyo ikizingatiwa kuwa aliwania wadhifa wa kisiasa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, na wala hakutengwa jinsi alivyodai.

Uamuzi huo unairuhusu serikali ya kaunti ya Bungoma kuendelea na mahojiano ya kuwateua wanachama wa bodi hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *