#Local News

NPS KIKAANGONI JUU YA MIRADI 4 ILIYOKWAMISHWA

Huduma ya Polisi ya Kitaifa (NPS) iko kwenye dhoruba baada ya ripoti ya Mhasibu Mkuu wa Taifa kuonyesha miradi minne iliyokwamishwa, pamoja na uvunjaji mkubwa wa mkataba na ukosefu wa uwajibikaji wa kifedha.

Akiwa mbele ya  Kamati ya Hesabu za Umma, Bernice Lemedeket ambaye ni afisa wa fedha wa NPS, alikosa kueleza ni kwa nini mradi wa jengo la ghorofa mbili lenye vyumba 24, lililokuwa limegharimu awali Shilingi milioni 64, ulirudiwa kwa kandarasi  ya Shilingi milioni 114.

Hii ni licha ya mkandarasi wa awali kulipwa Shilingi milioni 23 kwa mradi ambao ulikamilika asilimia 35 tu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *