WANAFUNZI 11 WAANGUKA NDANI YA SHIMO LA CHOO KAPSABET
Mwanafunzi mmoja amefariki na Wengine 10 wa Shule ya wasio na uwezo wa kusikia ya Kapsabet wamelazwa hospitalini baada ya kuanguka ndani ya shimo la choo lililoporomoka katika eneo la shule hiyo hilo wakati wanafunzi hao walipokuwa wakikimbilia kushuhudia msafara wa Rais William Ruto uliokuwa ukipita karibu na shule hiyo
Wanafunzi hao walikuwa wamesimama juu ya shimo hilo lenye urefu wa takribani futi 20 ambalo lilishindwa kuhimili uzito wao na kuporomoka.
Tukio hilo limethibitishwa na Afisa Mkuu wa Kaunti anayesimamia elimu katika Kaunti ya Nandi, Angeline Kirui, aliyekuwa miongoni mwa waokoaji wa kwanza kufika eneo la tukio huku Rais pia akibadili ratika kwa kifupi na kufika kwenye shule hiyo
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































