FAMILIA ZAACHIWA KUWASAKA WAPENDWA WAO
Shughuli za kuwasaka watu 10 wanaohofiwa kukwama kwenye udongo kufuatia maporomoko ya ardhi katika eneo la Chesongoch kaunti ya Elgeyo Marakwet zinaendelea huku serikali ikiratibu tarehe 21 mwezi huu kuwa siku ya kuwazika walioangamia.
Shughuli hizo zinaendelezwa na familia za waathiriwa na Wakazi, baada ya maafisa wa serikali kuondoka ikiwa ni wiki moja tangu kutokea kwa mkasa huo.
Watu 38 wamethibitishwa kufariki huku wengine 10 wakiwa hawajulikani waliko.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































