#Sports

STAGE 3 YA SAFARI RALLY YAFUTILIWA MBALI

Siku ya pili ya mashindano ya Safari Rally imetatizika mapema baada ya hatua ya 3 yaani Stage 3, SS3 Camp Moran ya mashindano hayo kufutiliwa mbali rasmi kutokana na hali mbaya ya barabara.

Kwa mujibu wa waraka karani wa mashindano hayo George Mwangi, uamuzi huo umechukuliwa kwa misingi ya usalama kufuatia kuharibika kwa barabara kutokana na matumizi mengi na kudorora kwa kiwango cha barabara.

Kutokana na kuondolewa kwa Camp Moran 2 kwenye orodha ya vituo vya waendesha magari kupitia, madereva sasa watapita moja kwa moja kuelekea Gilgil na Eburru, na kuibukia karibu na Malewa wakikwepa barabara kuu ya Nairobi kuelekea Naisha hadi Nakuru.

Baada ya mashindano hayo ya asubuhi, madereva watakongamana katika taasisi ya utafiti wa wanyamapori mjini Naivasha kabla ya kurejea uwanjani kupitia vituo vile vile.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *