GAVANA BARASA ATOA WITO WA UMOJA KWA VIONGOZI WA MAGHARIBI
Gavana wa Kaunti ya Kakamega, Fernandes Barasa, amewataka viongozi kutoka eneo la Magharibi mwa Kenya kuungana na kufanya kazi kwa mshikamano kwa maslahi ya wananchi.
Akizungumza katika kaunti ya Kakamega, Barasa amesisitiza kuwa umoja ndio njia sahihi ya maendeleo, akionya kuwa migawanyiko ya kisiasa na kijamii italeta vurugu na kusababisha kudorora kwa maendeleo katika eneo hilo.
Gavana huyo amesema kuwa ushirikiano miongoni mwa viongozi utasaidia kuimarisha amani, uthabiti na maendeleo endelevu kwa wakazi wa eneo la Magharibi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































